Ijumaa 13 Juni 2025 - 14:44
Mwanazuoni wa Kihindi: Ghadir ni mchoro wa ramani ya mwongozo wa Umma wa Kiislamu

Hawza/ Hujjatul-Islam Ali Haidar Fereshta, katika mahojiano na mwandishi wa habari wa Hawza, amesema kuwa Ghadir ni zaidi ya tangazo la urithi wa uongozi; ni mfano kamili wa mfumo wa uongozi wa Ki-Imam unaoongoza Umma wa Kiislamu. Amesisitiza pia haja ya kuunganisha ujumbe wa Ghadir na utamaduni wa Intidhār (kusubiri kwa matumaini) na maandalizi ya kudhihiri kwa Imamu wa Zama.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, haHujjatul-Islam Ali Haidar Fereshta, ambaye ni rais wa Jumuiya ya Maulamaa na makhatibu wa Hyderabad India, alisisitiza kuwa Eid al-Ghadir si sherehe ya kihistoria pekee, bali ni siku ya tangazo rasmi la mpango wa kina wa kimungu. Akirejea kwenye Qur'an Tukufu alisema:

«الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ، وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي، وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا»

Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini. (Sura al-Mā’ida, aya ya 3)

Siku ya Ghadir, kwa hakika, si siku ya kutangazwa wilaya tu, bali ni siku ya kukamilika kwa dini, ukamilifu wa neema ya Mwenyezi Mungu, na uthibitisho wa njia ya milele ya mwongozo kwa Umma wa Kiislamu.

Amesema kuwa; kuielewa Ghadir kama msingi wa mfumo wa Imāmah na Wilaya, na kufahamu ujumbe wake kwa kina, ndilo jambo kuu katika kuelewa ukweli wa sikukuu hii tukufu.

Juu ya dhana ya Wilaya ya Imam Ali (as):
Baadhi ya watu huiona Wilaya ya Imam Ali (as) kama tu fadhila ya kibinafsi, lakini Fereshta anasema mtazamo huo ni upotofu wa maana halisi ya Wilaya. Amesisitiza kwamba Wilaya ni mwendelezo wa kimaumbile na wa lazima wa njia ya Unabii, na ni sehemu ya pili ya mfumo wa mwongozo wa kimungu ambayo ina nafasi ya msingi katika kudumisha ujumbe wa Mwenyezimungu.

Kama jamii yoyote inavyohitaji mfumo wa kisiasa na wa haki ili iendelee na kudumisha uadilifu, vivyo hivyo dini ya Kiislamu inahitaji mfumo thabiti na wa kimungu ili kutimiza malengo yake ya juu, jambo ambalo linadhihirika kupitia taasisi ya Imāmah na Wilaya.

Imam Ali (as*) si tu shakhsia kubwa ya kihistoria, bali ni kipimo na mizani ya haki na batili. Kukataa wilaya yake ni sawa na kukataa njia ya mwongozo wa Mwenyezi Mungu. Hii ndiyo sababu katika hadithi za Ma’sumin (as), zinaonesha kuwa, kutengana na wilaya ni dalili ya unafiki na upotofu mkubwa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha